Friday, 29 December 2023

ZIFAHAMU BAADHI YA AYA ZA QURAAN ZINAZOHIMIZA AMANI NA MATENDO MEMA KWA BINADAMU WOTE

 



Ndugu wasomaji wangu karibuni katika Makala yetu ya leo ikielezea baadhi ya aya zinazohimiza amani na upendo. Katika Uislamu, Quraan ni maandiko matakatifu ambayo yanatoa mafundisho kwa waumini wa dini hiyo, katika maandiko hayo kuna baadhi ya aya ambazo zinatumika katika kusisitiza matendo ya amani kama ilivyo maana ya neno 'islamu', ambapo matendo hayo yanapelekea binadamu kuwa na mwisho mwema hapa duniani na akhera.

Vile vile uwepo kwa matendo hayo mema yanayopelekea kuwepo kwa amani na utulivu yatasaidia jamii kupata maendeleo.

Ili kuishi katika matendo hayo mema ni vyema kujifunza elimu ya dini ikiwemo Qur,ani, hadithi na sunna za mtume Muhammad (S.A.W).

Zifuatazo ni baadhi ya aya ambazo zinahimiza amani na matendo ya Amani katika dini ya kiislamu.

AYAYA8 katika SURAT MAIDAH, Aya hii inaeleza kuwa "Enyi waumini simameni imara kwaajili ya Mwenyezi Mungu na mchukue haki ushuhuda. Usiruhusu chuki ya watu ikupeleke kwenye dhulma. Kuwa mwadilifu, huko ndiko karibu na haki. Na mcheni Mwenyezi Mungu Hakika Mwenyezi Mungu anayo habari za mnayotenda". Lengo kuu la mafundisho ya aya hii ni kutenda haki na kutomtendea mtu mwengine mabaya bila kujali dini yake, kabila hata rangi.

Katika SURAT QAAF AYA 45, Aya hii imeeleza kuwa "Sisi tunajua Zaidi wanachosema na wewe Ewe Mtume si wakuwalazimisha kuamini, hivyo wakumbushe kwa quraan tu sio kuwalazimisha", lengo la aya hii kuhimiza matumizi sahihi ya quraani hasa katika kuwalingania watu na kutumia nguvu na vitisho kama wanavyofanya wanaharakati. Aya hii ikufuatwa ipasavyo itasaidia kuwepo kwa matendo ya amani ana utulivu katika jamii.

AYA YA 14 katika SURAT JATHIYAH, Aya hii imeeleza kuwa "Sema, Ewe Muhammed, kwa wale walioamini kwamba wawasamehe wale wasiotarajia siku za Mwenyezi Mungu, ili awalipe watu kwa yale waliyokuwa wakiyachuma " lengo la aya hii ni kuwa kwa mtu anayekosea haukumiwi na binaadamu mwenzie bali Mungu ndio anayetoa hukumu na endapo akatokea mtu au kikundi cha watu akahukumu watu wengine atakuwa ameenda kinyume na maamrishio ya Mwenyezi Mungu na Mtume Muhhammed (S.A.W)

Katika SURAT BAQARA AYA AYA 194, Aya hii imeeleza kuwa "kutakuwa na kisasi katika mwezi mtakatifu kwa kosa katika mwezi mtakatifu na ukiukwaji wote utaleta kisasi. Kwa hiyo, mtu akikushambulia, lipiza vivyo hivyo lakini kumbuka Mwenyezi Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yupo pamoja na wacha Mungu". Lengo la aya hii ni kuwa kazi ya kuhukumu aachiwe Mwenyezi Mungu, badala ya hukumu hiyo kufanywa na binaadamu dhidi ya binaadamu wenzao.

AYA 161 katika SURAT AL ANAFAL, Aya hii imeeleza kuwa "ikiwa adui ana mwelekeo wa amani, fanya amani nao. Na mtegemee Mwenyezi Mungu .Hakika yeye peke yake ndio mwenye kusikia, mjuzi wa yote " lengo la aya hii ni kusisitiza amani na utulivu miongoni mwa binaadamu wote na hukumu mwenye haki ya kutoa ni Mungu pekee.

Wito wangu kuwa elimu ni (mali, bahari, rasilimali, ufunguo wa maisha, ukombozi, uhai na fumbo la ujinga), hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa jamii kupata elimu ili kujikomboa kifikra na kuzuia watu wasiingie katika vitendo viovu katika jamii ambavyo vinaweza kuleta athari kubwa katika jamii.

Hata hivyo kuna umuhimu wa kusoma elimu (elimu ya dini) ili kupata maana sahihi za aya mbalimbali hasa zinazohimiza kuwepo kwa amani na utulivu, hali hilo itasaidia kuwepo kwa maendeleo katika jamii na Nchi kwa ujumla. Pia ufahamu wa aya hizo utasaidia kubaini watu ambao wanataka kutumia aya hizo kufanya upotoshaji kwa wengine.

No comments:

Post a Comment

MSAMAHA NA DHANA ZAKE

    Ndugu wasomaji karibuni katika Makala yetu ya leo ambayo inahusu jambo muhimu na msingi wa uwepo wa amani na utulivu katika maisha yetu...