Makala

NGUZO ZA KIISLAMU




Dini  hii ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo tatu za msingi, ambazo ni:-


1.  UISLAMU, ambao huu umejengwa juu ya nguzo     tano kama zifuatavyo:-

                Shahada mbili
                Kusimamisha swala tano
                Kutoa zakah
                Saumu ya Ramadhani
                Kuhiji Makah (kwa mwenye uwezo).


2.         IMANI nguzo hii  ya pili ya dini ya Kiislamu inajengeka juu ya nguzo sita                         zifuatazo:-

i.      Kumuamini  Allah

ii.     Kuwaamini malaika wa Allah.

iii.    Kuviamini vitabu vya Allah.

iv.    Kuwaamini mitume (wote ) wa Allah.
v.     Kuamini siku ya mwisho.
vi.    Kuamini qadari ya Allah (ya kheri au ya shari) kuwa inatoka kwa Allah).


3.         IHSANI. Nguzo hii ya tatu inaundwa na nguzo hii:-

            Kumuabudu Allah kama unamuona Kama humuoni yeye anakuona wewe.

            Huu kwa muhtasari ndio Uislamu, dini na mfumo sahihi na kamili wa maisha

                 kwa wanadamu wote waliochaguliwa na Allah Mola Muumba wao:

                “………LEO NIMEKUKAMILISHENI DINI YENU NA KUKUTIMIZIENI                             NEEMA YANGU NA NIMEKUPENDELEENI UISLAMU UWE DINI         YENU            ………….” (5:3)


        Elewa na ufahamu kwamba kuishi nje ya dini hii ni kulikana umbile lako kwani            UISLAMU NI HAKI YAKO YA KUZALIWA uliyopewa hadiya (zawadi) na                        Mola Muumba wako.

        Endelea kuungana nasi katika mafundisho yajayo............. 

No comments:

Post a Comment

MSAMAHA NA DHANA ZAKE

    Ndugu wasomaji karibuni katika Makala yetu ya leo ambayo inahusu jambo muhimu na msingi wa uwepo wa amani na utulivu katika maisha yetu...