Sheikh
wa mkoa wa Manyara Alhaj Sheikh Muhamad Khamis Kadidi kwa niaba ya Waislamu
mkoani humo ametoa pole kwa wahanga wa Mafuriko wilaya ya Hanang' akiwataka
kuwa watulivu na Subra katika kipindi hiki kigumu.
Aidha Sheikh wa Mkoa amewaagiza Viongozi wa Baraza kuanzia Mkoa, Wilaya , Kata, Misikiti na Jumuiya zote za Baraza kwa maana ya Jumuiya ya Vijana (JUVIKIBA) na Jumuiya ya Kina mama (JUWAKITA) kutoa Msaada kwa wahanga wote na Misikiti na majengo yote ya Baraza kutumika katika kutoa Msaada katika kipindi hichi.
Sheik
Kadidi anawaombea Marehemu wote Allah aziweke Roho zao Mahala pema pamoja na
kuwaombea majeruhi wote Allah awaponye haraka na kuwarejesha kwenye
Shughuli zao za kawaida.
.png)
No comments:
Post a Comment